Karibuni

Ikiwa bado uko chini ya uongozi wa Mashirika Ya Kutoa Misaada Ya Kikatoliki, wasiliana na msimamizi wako wa kesi ili kupata msaada kuhusu mojawapo ya maswali haya.

JE, NAPASWA KUMPIGIA NANI SIMU NYUMBA AU KWENYE FLETI YANGU IKIWA NA MATATIZO?

Unapokodisha nyumba au fleti, unatia sahihi mkataba wa kukodisha unaohitaji uishi hapo kwa muda fulani. Ikiwa nyumba yako ina matatizo, wasiliana na mwenye nyumba au uwakala wa kukodisha.


JE, NAPASWA KUMPIGIA NANI SIMU KUHUSU HUDUMA YANGU YA UMEME, MAJI AU GESI?

Bili ya umeme: Kampuni ya Alabama Power

Bili ya Maji: Kampuni ya Mobile Area Water and Sewer System

Bili ya Gesi: Welcome Mobile Gas Customers


JE, NITAPATA USAIDIZI VIPI KUHUSU KUNUNUA CHAKULA?

Mpango wa SNAP

WIC


JE, NAPASWA KUFANYA NINI ENDAPO MIMI AU WATOTO WANGU TUTAUGUA?

Ikiwa una Medicaid, wasiliana na KidsStreet Urgent Care Mobile - Kliniki ya Pediatric Urgent Care Hufunguliwa Hadi Usiku

Ikiwa ni dharura, nenda kwenye chumba cha dharura.

Ikiwa unahitaji gari la kubebea wagonjwa, piga simu kwa 911.

 

JE, NAPASWA KUFANYA NINI NIKISHINDWA KWENDA KAZINI?

Unapaswa kumpigia simu mwajiri wako mapema iwezekanavyo ikiwa huwezi kwenda kazini.


JE, NITAWASILIANA VIPI NA SHULE YA WATOTO WANGU?

Unaweza kupata nambari ya simu ya shule ya mtoto wako kwenye tovuti hii.


NINAWEZA KUWAACHA WATOTO WANGU NYUMBANI PEKE YAO?

Ni muhimu kuwa na usimamizi wa kutosha kwa watoto wadogo ambao wako nyumbani. 


NINAPASWA KUFANYA NINI, NIKISIMAMISHWA NA POLISI NINAPOENDESHA GARI?

Egesha gari kando ya barabara na usubiri afisa huyo aje kwenye dirisha lako.

Wakati wote, weka mikono yako mahali ambapo inaweza kuonekana na usitoroke.


UNA MASWALI MENGINE AU UNAHITAJI USAIDIZI ZAIDI?

Wasiliana nasi.